Shule ya msingi Darpori kitabu kimoja wanasoma darasa zima

Standard

Picha inawaonesha wanafunzi wa darasa la tatu na la nne katika shule ya msingi Darpori wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakiwa wanasomea katika chumba kimoja cha darasa kwa wakati mmoja jambo ambalo linaleta usumbufu mkubwa katika tendo la kujifunza na kufundisha.
  

Na Albano Midelo

ELIMU bora kwa watanzania wote wa mjini na wale wanaoishi katika mazingira magumu hapa nchini  ni moja ya malengo ya millennia ya serikali ya chama tawala  ndiyo maana ulianzishwa mpango wa kuboresha elimu ya msingi MEM na kuboresha elimu ya sekondari MES.

Hata hivyo mpango wa kuboresha elimu bora kwa watanzania unaonekana kukabiliwa na changamoto nyingi katika baadhi ya maeneo yenye mazingira magumu kama hali ilivyo katika shule ya msingi Darpori iliyopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma. Mwenyekiti wa kijiji cha Darpori Andason Haule anasema kijiji hicho chenye utajiri wa madini ya dhahabu kina watu karibu 10,000 kilianza rasmi mwaka 2004, kina karibu makabila yote 120 yaliopo nchini pamoja raia kutoka nchi jirani za Malawi na Msumbiji. Read the rest of this entry

Advertisements

Ugonjwa wa kifafa washambulia kijiji kizima

Standard

   Picha inamunesha mwanafunzi wa shule ya msingi Mtua iliyopo katika kata ya Mpepai wilayani Mbinga mkoani Ruvuma akiwa ameungua moto.Mwanafunzi huyu anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa,alipata ajali ya moto baada ya ugonjwa huo kumuanza akiwa hata mwangalizi hivyo kuangukia kwenye moto

Na Albano Midelo

Wananchi wa Kijiji cha Mtua ambacho kinapakana na pori la wanyamapori la Liparamba wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wapo katika hatari baada ya ugonjwa wa kifafa kushambulia karibu kijiji kizima.

Uchunguzi umebaini kuwa  katika kijiji hicho chenye wakazi zaidi ya 1600 watu 200 wanadaiwa wanaugua kifafa ambapo kila nyumba kuna mgonjwa mmoja wa kifafa na baadhi ya nyumba zina wagonjwa wawili hadi watatu hali ambayo inasababisha wananchi wa kijiji hicho kuhitaji msaada mkubwa kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa lengo la kukinusuri kijiji hicho. Read the rest of this entry

Ubovu wa barabara wasababisha nauli kufikia 40,000

Standard


Picha inawaonesha wasafiri wanaotoka wilayani Mbinga kwenda kijiji cha Darpori kilichopo mpakani  mwa Tanzania na Msumbiji  ambao licha ya kulipa nauli ya shilingi 40,000 pia wanakaa juu ya magari au kushika bomba kama wanavyoonekana katika picha  

  Na Albano Midelo.

UBOVU wa barabara  yenye urefu kilometa 82 kutoka wilayani Mbinga hadi katika kijiji cha Darpori kilichopo mpakani mwa  nchi za Tanzania na Msumbiji kumesababisha abiria kulipa nauli kati ya shilingi 30,000 hadi 40,000.

Uchunguzi ambao umefanywa na mwandishi wa habari hizi  umebaini kuwa wananchi wanaoishi katika kijiji hicho na kilichopo katika kata ya Tingi wanakabiliwa na matatizo makubwa yanayotokana na tatizo sugu la ubovu wa barabara. Read the rest of this entry

Mwekezaji apora eka 5000 za wananchi

Standard


Picha inaonesha baadhi ya wakulima katika kijiji cha Lipokela wilayani Songea wakivuna mahindi yao baada ya kuwaambiwa kuwa mashamba hayo sio mali yao ni mali ya mwekezaji hivyo wanatakiwa wayavune haraka.

Na Albano Midelo

WAKAZI wa kijiji cha Lipokela wilayani Songea mkoani Ruvuma  wanamuomba waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi  Profesa Anna Tibaijuka kuwasaidia kuirejea ardhi yao yenye ukubwa wa zaidi ya eka 5000  iliyochukuliwa kinyemela na mwekezaji.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika kijiji hicho baadhi ya wananchi walidai kuwa  mwekezaji mwenye asili ya Asia anayefahamika kwa jina moja la Merali  tangu mwaka 1985 alipewa ardhi kinyemela bila Baraka za wananchi na kusababisha ardhi hiyo kuingia kwenye mgogoro mkubwa. Read the rest of this entry

Mimba zinavyotishia elimu kwa wanafunzi Ruvuma

Standard

Na Albano Midelo.

 JUMLA ya wanafunzi 554  wamepata mimba katika mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka jana. Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dr.Christine Ishengoma alibainisha kuwa kati ya waliopewa mimba  wanafunzi wa shule za msingi ni 283 na sekondari 271.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa kati hao waliopewa mimba wilaya ya Mbinga wanafunzi 114 wakiwemo wa shule za msingi 15 na sekondari 99 walitiwa mimba ambapo kesi tatu zipo mahakamani na kesi 111 zipo katika ofisi za watendaji wa vijiji.Wilaya ya Namtumbo wanafunzi 148 ,kati ya hao wanafunzi wa shule za msingi 106 na sekondari 42 ambapo mahakamani zipo kesi 21,polisi kwa ajili ya upelelezi zipo kesi 28,ofisi za watendaji wa vijiji kesi 43 na kesi 14 zipo katika ofisi za watendaji wa kata. Read the rest of this entry