Mchawi wa umeme Songea abainika

Standard

 

Mashine mpya aina ya ABC ambayo ilitolewa katika ahadi za Rais Jakaya Kikwete tayari imefungwa kwa lengo la kupunguza tatizo la umeme mjini Songea.Mashine hiyo ina uwezo wa kuzalisha megawati 1.6

Na Albano Midelo

UBOVU wa mashine tatu kati ya sita za kuzalishia umeme katika kituo cha TANESCO mjini Songea mkoani Ruvuma umesababisha mgawo mkali wa umeme kwa wakazi wa mji huo.

Uchunguzi umebaini kuwa mgawo wa umeme umesababisha kazi za kiuchumi kushindwa kufanyika na kusababisha baadhi ya wananchi wenye uwezo kuamua kutumia majenereta madogo huku maeneo mengi ya mji wakati wa usiku yakiwa giza kwa saa kadhaa.

Kaimu mkuu wa kituo cha kuzalishia umeme TANESCO Songea injinia Isaack Mbata akizungumzia tatizo la mgawo wa umeme alisema linasababishwa na ubovu wa mashine tatu zenye uwezo wa kuzalisha megawati 3.2 ambazo hazifanyikazi. Alisema mashine tatu zinazozalisha umeme hivi sasa katika mji wa Songea zina uwezo wa kuzalisha megawati 2.2 ambapo mahitaji halisi ya umeme katika mji wa Songea ni megawati 4.5 . “Umeme unaozalishwa hivi sasa ni karibu nusu ya mahitaji ya umeme katika mji wa Songea ,hali hii imesababisha kuwepo mgawo mkali wa umeme,hata hivyo mashine tatu ambazo ni mbovu vipuli vyake vimeagizwa na TANESCO makao makuu vikiletwa tutavifunga mara moja na umeme utarudi katika hali yake ya kawaida’’,alisema injinia Mbata. Naye kaimu meneja wa TANESCO mkoa wa Ruvuma Haruna Mwachula amewaomba wakazi wa mji wa Songea kuwa wavumilivu katika kipindi hiki ambacho shirika hilo linafanya juhudi za kutengeneza mashine mbovu tatu ili kupunguza mgawo mkali wa umeme uliopo. Alisisitiza kuwa mafundi wa TANESCO wanafanyakazi usiku na mchana ambapo tayari wamefanikiwa kufungua vipuli vyote vibovu kwenye mashine aina ya katapila na ABC zenye uwezo wa kuzalisha megawati 3.2 Hata hivyo Mwachula alibainisha kuwa mashine mpya aina ya ABC yenye uwezo wa kuzalisha megawati 1.6 ambayo ilitolewa kwa ahadi ya Rais Jakaya Kikwete tayari imefungwa na inafanyakazi ikisaidiwa na mashine mbili za zamani aina ya wartisila zenye uwezo wa kuzalisha kilowati 800. “Kazi ya kufunga vipuli katika mashine tatu ikikamilika itawezesha mashine zote kuzalisha umeme wa megawati 5.5 wakati mahitaji katika mji wa Songea ni megawati 4.5 hivyo kupatikana kwa umeme wa ziada na tatizo la mgawo wa umeme kubakia kuwa historia’’,alisisitiza. Kuhusu mafuta ya kuendeshea mashine hizo ,Mwachula alisema mafuta yapo ya kutosha kukidhi mahitaji ya kuendeshea mashine za umeme na amekanusha uvumi ulioenea mjini Songea kuwa mgawo wa umeme uliopo unatokana na uhaba wa mafuta. Mwisho.

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s