Wanawake 960 wafanyiwa ukatili Ruvuma

Standard

Mwanaharakati Fatuma Misango katikati akisikiliza  baadhi ya wanawake wakielezea ukatili wanaofanyiwa na wanaume zao.

Na Albano Midelo

MWANAHARAKATI wa haki za wanawake na watoto katika mkoa wa Ruvuma Fatuma Misango anasema takwimu za wanawake na watoto wanaofanyiwa vitendo vya ukatili mkoani humu vinatishia ustawi wa jamii.

Misango ambaye pia ni mratibu wa kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto( WLAC) mkoani humo anasema kwa mwaka 2010 pekee kituo hicho kilifikiwa na wanawake 960 wa mkoa huo ambao walikuwa wananyanyaswa na kuhitaji msaada wa kisheria. Misango alibainisha kuwa wanawake hao walikuwa na migogoro katika familia zao kuhusiana na ndoa,mirathi na migogoro ya ardhi na kwamba kituo chake kimekuwa kinawatetea zaidi wanawake kutokana na ubabe wa wanaume walio wengi. Hata hivyo alikiri kuwa wapo wanawake ambao wanawanyanyasa waume zao ambao pia amekuwa anakutana nao na kuwapatia ushauri,ingawa alisema idadi ya wanaume wanaonyanyaswa na wanawake ni wachache. “Mwanaume mmoja alisimulia namna anavyonyanyaswa na mkewe kwenye ndoa,kwamba mke alikuwa mlevi na anarudi nyumbani usiku bila kujali kuwahudumia watoto,hii inaonesha kuwa unyanyasaji upo kwa wote ‘’anasema. Hata hivyo Misango anasema kituo chake pia kimekuwa kinafuatilia hali za watoto hasa wale ambao wamekuwa wananyanyaswa na kukosa haki zao za msingi, “Moja ya kesi ambazo zilinisikitisha ni ya mtoto wa miaka 16 alihukumiwa kwenda jela miaka mitano kwa kosa la kuiba sabuni kipande kimoja,tulikata rufaa ili haki iangaliwe upya,tulibaini kuwa kesi hiyo alibambikizwa,tulishinda kesi,mtoto akatoka gerezani na hivi sasa yupo katika kijiji cha Hanga wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma’’,anasema. Anabainisha kuwa kituo chake kimekuwa kinawatetea wanawake na watoto wengi kwa kushirikiana na wanasheria mbalimbali wanawake na kwamba harakati za kutetea haki za wanawake na watoto zilimwezesha mwaka 2005 kupata tuzo ya Nobel akiwa ni miongoni mwa wanawake 1000 waliopata tuzo hiyo duniani. “Nchi 156 mwaka 2005 zilipewa tuzo kupitia wanawake waliokuwa mstari wa mbele kutetea wanawake na watoto,Tanzania tulikuwa wanawake watatu ambao tulipewa tuzo hiyo,mimi nikiwa miongoni mwa wanawake hao waliobahatika kupata tuzo inaitwa 1000 piece Woman Across The Global’’,anasisitiza. Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa inakadiriwa kuwa asilimia 60 ya wanawake duniani wamepitia dhuluma na ukatili wa aina mbalimbali hasa kwa kupigwa na waume zao. Albano.midelo@gmail.com,simu

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s