Monthly Archives: February 2012

Mchawi wa umeme Songea abainika

Standard

 

Mashine mpya aina ya ABC ambayo ilitolewa katika ahadi za Rais Jakaya Kikwete tayari imefungwa kwa lengo la kupunguza tatizo la umeme mjini Songea.Mashine hiyo ina uwezo wa kuzalisha megawati 1.6

Na Albano Midelo

UBOVU wa mashine tatu kati ya sita za kuzalishia umeme katika kituo cha TANESCO mjini Songea mkoani Ruvuma umesababisha mgawo mkali wa umeme kwa wakazi wa mji huo.

Uchunguzi umebaini kuwa mgawo wa umeme umesababisha kazi za kiuchumi kushindwa kufanyika na kusababisha baadhi ya wananchi wenye uwezo kuamua kutumia majenereta madogo huku maeneo mengi ya mji wakati wa usiku yakiwa giza kwa saa kadhaa. Read the rest of this entry

Advertisements

Wanawake 960 wafanyiwa ukatili Ruvuma

Standard

Mwanaharakati Fatuma Misango katikati akisikiliza  baadhi ya wanawake wakielezea ukatili wanaofanyiwa na wanaume zao.

Na Albano Midelo

MWANAHARAKATI wa haki za wanawake na watoto katika mkoa wa Ruvuma Fatuma Misango anasema takwimu za wanawake na watoto wanaofanyiwa vitendo vya ukatili mkoani humu vinatishia ustawi wa jamii.

Misango ambaye pia ni mratibu wa kituo cha msaada wa kisheria kwa wanawake na watoto( WLAC) mkoani humo anasema kwa mwaka 2010 pekee kituo hicho kilifikiwa na wanawake 960 wa mkoa huo ambao walikuwa wananyanyaswa na kuhitaji msaada wa kisheria. Read the rest of this entry