Wanakijiji Mbinga wahofia kutoroshwa kwa makaa ya mawe

Standard
  Makaa ya mawe ya kijiji  cha Liyombo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.Na Albano Midelo

WANANCHI wa kijiji cha Liyombo kata ya Ruanda wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wameonyesha wasiwasi wao juu ya kudaiwa kutoroshwa kwa makaa ya mawe pamoja na ulipwaji wa  fidia watakazo pata kwa mali zao,baada ya kufahamika kuwa kijiji hicho kimejengwa juu ya mwamba wa makaa ya mawe ambayo yanatarajiwa kuanza kuchimbwa kabla ya mwisho wa mwaka huu iwapo taratibu za vibali kwa mwekezaji zitakamilika.

Baadhi ya wakazi  wa  kijiji hicho kilichopo katika kata ya Ruanda ambao ni Elia Hyera,John Mbepera na Joakimu Nchimbi wakizungumzia suala hilo wametoa wito kwa serikali kusimamia na kuhakikisha wanalipwa fidia pamoja na kuwa makini na kufuatilia sampuli za makaa hayo zinazopelekwa nje ya nchi kwa madai ya kwenda kufanya utafiti wa ubora wa makaa ya mawe kabla ya kuanza kuchimbwa.

“Hawa wawekezaji wamechukua sampuri tani 1000 na kupeleka nchini Afrika ya kusini kwa njia ya ,meli kupitia bandari ya Ndumbi ziwa Nyasa, kwa ajili ya utafiti wa awali,halafu wanasema bado zinatakiwa tani 10,000 ili kukamilisha utafiti na kuwaridhisha wanunuzi wa makaa hayo nje ya nchi,sisi wananchi wanatuchanganya mara wanasema majibu yanaonyesha kuwa mkaa huo ni bora hatujui tena tani nyingine za nini,wizara ya madini inatakiwa kusimamia hali hii isije ikiwa ni janja ya nyani’’,alitahadharisha Elia Hyera.

Kampuni ya Tancoal Energy Limited (TANCOAL) , shirika la Taifa la maendeleo ( NDC), pamoja  na Pacific Corporation ya Afrika Mashariki (PCAM), walianza utafiti wa kuchimba makaa ya mawe katika  kijiji cha Liyombo ambapo utafiti umebaini eneo hilo kuwa na mkaa wa kutosha  na wenye ubora.Utafiti huo ulianza  April mwaka 2008 kwa kuangalia wingi wa makaa ya mawe,unene wa mwamba na ubora wa makaa hayo.

Utafiti ambao umefanyika katika kijiji hicho kwa miaka minne sasa umebaini kuwa kijiji cha Liyombo kipo juu ya mwamba bora wa makaa ya mawe ambapo Meneja wa uchimbaji ya TANCOAL ambayo ina hisa ya asilimia 70  Gordon Mc Cormack,alisema kuwa  mwelekeo wa kazi hiyo ni kupata nishati ya kutosha itakayo saidia uchumi wa mkoa wa Ruvuma na Taifa kwa ujumla.

Alibainisha kuwa mgodi huo unatarajia kuwa chanzo kikubwa cha utoaji wa makaa ya mawe hapa nchini na kusambaza kwa wahitaji wote wa nishati hiyo hapa nchini vikiwemo viwanda na nje ya nchi na kwamba kitakuwa chanzo kikuu cha umeme kimataifa na msaada katika gridi  ya umeme ya taifa ambayo hivi  sasa umeme wake hautoshelezi na kusababisha mkali wa umeme mgawo.

Mtaalamu wa miamba Alex Sostenes alibainisha zaidi kuwa   makaa hayo ya mawe yamesambaa maeneo yote ya Ngaka na Liyombo pamoja na maeneo mengine  ya jirani  na kijiji cha Liyombo na kwamba mashine ya utafiti kwa utalaamu itatoboa shimo moja kijijini hapo ili kubaini wingi wa mkaa na ubora wake na kuwataka wanakijiji wasiwe na wasiwasi juu ya nyumba zao ama mali zao.

Hata hivyo mkurugenzi mkuu wa TANCOAL  Emmanuel Costantinides  amethibitisha kuwa  mkaa wa mawe wa kijiji cha Liyombo ni mkaa bora kutokana na majibu ya “ sampuri zilizopelekwa Afrika Kusini kwa uchunguzi kupitia Bandari ya Ndumbi Ziwa Nyasa.

“Kiasi cha tani 1000 zimesafirishwa kupelekewa nchini Afrika ya kusini kwa uchunguzi wa awali kwa madhumuni ya kujiridhisha ambapo matokeo yameonyesha dalili nzuri kwa kuwa mkaa unaonyesha  ubora wake haufanani na mkaa wa mawe unaochimbwa katika nchi yeyote duniani,mkaa wa Mbinga  ni bora kuliko mikaa mingine yote duniani’’,alisisitiza.

Hata hivyo alisema  bado tani 10,000  zinahitajika  kupelekwa nchini Afrika ya kusini  kama sampuri kutoka eneo la utafiti ili wanunuzi waweze kujiridhisha zaidi ingawa hali hiyo inaleta hofu kwa wakazi wa kijiji hicho ambao wanashauri ni bora utafiti ungefanyika hapa hapa nchini ili kusifanyike hujuma ya kusafirisha maliasili nje ya nchi kwa kisingizio cha utafiti huku watanzania wakibakia kuambulia mashimo kutokana na uharibifu wa mazingira.

Mgodi wa makaa ya mawe ya Liyomba na  Ngaka wilayani Mbinga umekadiriwa kuwa na zaidi ya tani 400 milioni za mkaa wa mawe. Kiasi hicho, kwa mujibu wa wataalam, kinaweza kuchimbwa kwa kipindi cha zaidi ya miaka 100.

Hata hivyo sera Taifa ya madini ya mwaka 1997 inasisitiza juu ya sekta binafsi kuendeleza madini, na wakati huo huo Serikali ikiwa na jukumu la kuidhibiti, kuikuza, kuiwezesha  na kuiendelea.Sekta ya madini inachangia takribani asilimia 2.3 ya pato la Taifa, ambayo inakadiriwa kufikia asilimia 10 ifikapo 2025.

Kwa mawasiliano andika albano.midelo@gmail.com,simu 0766463129

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s