Monthly Archives: September 2011

Mtalii sasa anaweza kutembea kwa miguu hifadhi ya Taifa Mikumi

Standard

 

Na Albano Midelo.

HIFADHI zilizo nyingi za  wanyamapori zilizopo hapa nchini watalii wanaruhusiwa kuangalia wanyama  wakiwa ndani ya magari ya kubeba watalii kuhofia kushambuliwa na wanyama wakali kama simba,tembo faru au chui pamoja na wanyamapori wengine.

Hata hivyo hali ni tofauti kabisa katika hifadhi ya Taifa ya mikumi iliyopo mkoani Morogoro yenye wanyama wenye mvuto wa kipekee ambao wengi wanawafurahia kuwaona hata wanapopita katika barabara kuu ya Iringa Dar es salaam ambayo inapita kwenye hifadhi ya Mikumi. Read the rest of this entry

Advertisements

Wanakijiji Mbinga wahofia kutoroshwa kwa makaa ya mawe

Standard
  Makaa ya mawe ya kijiji  cha Liyombo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.Na Albano Midelo

WANANCHI wa kijiji cha Liyombo kata ya Ruanda wilaya ya Mbinga mkoani Ruvuma wameonyesha wasiwasi wao juu ya kudaiwa kutoroshwa kwa makaa ya mawe pamoja na ulipwaji wa  fidia watakazo pata kwa mali zao,baada ya kufahamika kuwa kijiji hicho kimejengwa juu ya mwamba wa makaa ya mawe ambayo yanatarajiwa kuanza kuchimbwa kabla ya mwisho wa mwaka huu iwapo taratibu za vibali kwa mwekezaji zitakamilika.

Baadhi ya wakazi  wa  kijiji hicho kilichopo katika kata ya Ruanda ambao ni Elia Hyera,John Mbepera na Joakimu Nchimbi wakizungumzia suala hilo wametoa wito kwa serikali kusimamia na kuhakikisha wanalipwa fidia pamoja na kuwa makini na kufuatilia sampuli za makaa hayo zinazopelekwa nje ya nchi kwa madai ya kwenda kufanya utafiti wa ubora wa makaa ya mawe kabla ya kuanza kuchimbwa. Read the rest of this entry