TACRI kanda ya kusini kuzalisha mamilioni ya miche bora ya kahawa

Standard

Picha inawaonesha baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya utafiti wa zao la kahawa Tanzania TACRI wakitoe elimu ya miche bora ya kahawa ya chotara yenye uwezo wa kutoa mazao mengi na haishambuliwi na magonjwa kwa urahisi.

Na Albano midelo.

TAASISI ya utafiti wa zao la kahawa Tanzania TACRI katika kituo cha Ugano wilayani  Mbinga mkoani Ruvuma kimeweza kuzalisha miche bora ya kahawa milioni 14  katika kipindi cha miaka kumi sasa.

Mkuu wa TACRI katika kituo cha Ugano kanda ya kusini Godbless Shao  aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa kuwa wakati Taasisi hiyo Septemba tisa mwaka huu inaadhimisha Jubilei ya miaka kumi tangu kuanza kazi ya utafiti wa zao la kahawa nchini iliyoanza rasmi mwaka 2001 ambapo katika kituo kikuu cha utafiti cha Liamungo wilayani Moshi TACRI inaazimisha miaka 77 ya utafiti wa zao la kahawa Tanzania.

Shao alibainisha kuwa  TACRI imeweza kupata mafanikio makubwa yaliosababisha wakulima kuzalisha aina kumi mpya za kahawa bora  aina ya arabika yenye uwezo wa kutoambukizwa magonjwa ya mimea kwa urahisi na kwamba tayari miche aina ya chotara yenye uwezo wa kutoa mazao mengi imepelekwa kwa wakulima  wa kahawa kanda ya kusini.

     Picha inaonesha aina ya mche wa chotara wenye uwezo wa kuzalisha kahawa nyingi pamoja na kutoshambuliwa kwa urahisi na magonjwa ya kahawa.Mche huu unazalishwa na TACRI na kusambazwa kwa wakulima wa kahawa katika mikoa ya Ruvuma na Iringa.

“Kabla ya TACRI kueneza miche bora ya kahawa  kulikuwa na magonjwa aina ya chulebuni pamoja na ugonjwa wa kutu ya majani magonjwa haya awali yalikuwa ni vigumu kuyadhibiti kwa kuwa madawa yake aina ya kopa gharama za uzalishaji zilikuwa zimepanda kwa asilimia kati ya 30 hadi 50 ,kugundulika kwa miche hiyo chotara kumeleta mapinduzi makubwa ya uzalishaji wa kahawa katika ukanda wa kusini ‘’,alisema.

Alibainisha kuwa TACRI katika kanda ya kusini imeweza kusambaza miche bora ya kahawa katika wilaya za Ludewa,Kilolo,Njombe,Makete,Mufindi,Iringa vijijini katika mkoa wa Ruvuma na katika mikoa wa Ruvuma miche hiyo imesambazwa katika wilaya za Mbinga na Songea.

Kwa mujibu wa Shao katika kipindi cha miaka kumi TACRI imeweza kusambaza teknolojia ya mafunzo kwa wakulima wapatao 43,000 katika kanda ya kusini na kwamba wakulima wa kahawa wameipokea teknolojia hiyo iliongeza ubora wa daraja kutoka17 hadi tisa  na kufikia daraja  saba hadi la nne hivi sasa na kwamba kutokana na ubora wa kahawa bei katika soko imekuwa inaongezeka na mwaka huu kilo itakuwa inauzwa kati ya shilingi 4500 hadi 5000 kwa kilo .

Hata hivyo aliitaja changamoto ambayo ilikuwa inakikabili kituo hicho cha utafiti tangu mwaka 2007  ni kuzuka kwa wadudu aina ya  vidung’ata ambao walikuwa wanashambulia kahawa hali iliyosababisha mazao kupungua na kwamba kituo hicho katika msimu huu kimefanikiwa kumaliza tatizo hilo kwa kushirikiana na Halmashauri ya wilaya ya Mbinga  ambapo hivi sasa ugonjwa huo umebakia kuwa ni historia.

Matarajio ya TACRI katika kipindi cha miaka kumi ijayo ni kuongeza uzalishaji wa kahawa katika kanda ya kusini  kutoka miche milioni 14 hadi kufikia milioni 55 na kitaifa kufikia uzalishaji wa miche milioni 200.

Kwa mawasiliano andika albano.midelo@gmail.com

Advertisements

Leave a Reply

Fill in your details below or click an icon to log in:

WordPress.com Logo

You are commenting using your WordPress.com account. Log Out /  Change )

Google+ photo

You are commenting using your Google+ account. Log Out /  Change )

Twitter picture

You are commenting using your Twitter account. Log Out /  Change )

Facebook photo

You are commenting using your Facebook account. Log Out /  Change )

w

Connecting to %s