Monthly Archives: August 2011

Mtoto atelekezwa na wazazi baada ya kuzaliwa na ulemavu wa haja kubwa

Standard

   Mtoto Anna Mapunda mwenye umri wa miaka mitatu mkazi wa kijiji cha Mkako wilayani Mbinga mkoani Ruvuma akiwa na mlezi wake Veronika Milanzi ambaye ni katibu wa kanisa la TAG Ruhuwiko Songea  baada ya kutelekezwa na wazazi wake wote wawili baada ya kuzaliwa na ulemavu katika njia ya haja kubwa

Na Albano Midelo

MTOTO Anna Mapunda mwenye umri wa miaka mitatu  mkazi wa kijiji cha Mkako wilayani Mbinga mkoani Ruvuma anahitaji msaada wa matibabu katika hospitali ya Muhimbili jijini Dar es salaam baada ya kuzaliwa na ulemavu sehemu ya haja kubwa.

Mtoto huyo anasumbuliwa na tatizo la kutokwa na sehemu ya haja kubwa nje kila anapokwenda kujisaidia na kwamba sehemu hiyo hukaa nje kwa hadi saa tatu kisha huanza kurudi yenyewe taratibu ambapo mtoto huyo hupata maumivu makali. Read the rest of this entry

Advertisements

TACRI kanda ya kusini kuzalisha mamilioni ya miche bora ya kahawa

Standard

Picha inawaonesha baadhi ya wafanyakazi wa Taasisi ya utafiti wa zao la kahawa Tanzania TACRI wakitoe elimu ya miche bora ya kahawa ya chotara yenye uwezo wa kutoa mazao mengi na haishambuliwi na magonjwa kwa urahisi.

Na Albano midelo.

TAASISI ya utafiti wa zao la kahawa Tanzania TACRI katika kituo cha Ugano wilayani  Mbinga mkoani Ruvuma kimeweza kuzalisha miche bora ya kahawa milioni 14  katika kipindi cha miaka kumi sasa.

Mkuu wa TACRI katika kituo cha Ugano kanda ya kusini Godbless Shao  aliwaambia waandishi wa habari mjini hapa kuwa wakati Taasisi hiyo Septemba tisa mwaka huu inaadhimisha Jubilei ya miaka kumi tangu kuanza kazi ya utafiti wa zao la kahawa nchini iliyoanza rasmi mwaka 2001 ambapo katika kituo kikuu cha utafiti cha Liamungo wilayani Moshi TACRI inaazimisha miaka 77 ya utafiti wa zao la kahawa Tanzania. Read the rest of this entry

Darpori kijiji chenye watu 10,000 ambacho hakina huduma ya afya tangu uhuru

Standard

Picha inakionesha kijiji cha Darpori kilichopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma,kijiji hiki kina watu 10,000 kipo mpakani mwa nchi za Tanzania na Msumbiji,tangu uhuru hadi sasa kijiji hiki licha ya kuwa na utajiri wa milima yenye dhahabu na idadi kubwa ya watu hakina huduma yeyote ya afya hali ambayo inaathiri ustawi wa jamii ikiwa ni pamoja na watu kupoteza maisha. 

-Wajawazito wanasafiri kilometa 18 kufuata huduma ya uzazi

Na Albano Midelo

WAHENGA walisema tembea uone mambo,ndivyo nilivyofanya mimi kufunga safari kutoka mjini Songea hadi kufika katika kijiji cha Darpori wilayani Mbinga mkoani Ruvuma umbali wa  takribani kilometa 200.

Kijiji cha Darpori kipo mpakani mwa Tanzania na nchi ya Msumbiji ,kutoka katika kijiji hicho kueleka nchini Msumbiji kwa mguu ni dakika 60,wakazi wa kijiji hiki ni wageni ambao wamefika katika kijiji hicho kwa ajili ya kufanyakazi ya uchimbaji na ununuzi wa madini mbalimbali yakiwemo  dhahabu ambayo yanapatikana kwa wingi katika kijiji hicho. Read the rest of this entry

Shule ya msingi Darpori kitabu kimoja wanasoma darasa zima

Standard

Picha inawaonesha wanafunzi wa darasa la tatu na la nne katika shule ya msingi Darpori wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wakiwa wanasomea katika chumba kimoja cha darasa kwa wakati mmoja jambo ambalo linaleta usumbufu mkubwa katika tendo la kujifunza na kufundisha.
  

Na Albano Midelo

ELIMU bora kwa watanzania wote wa mjini na wale wanaoishi katika mazingira magumu hapa nchini  ni moja ya malengo ya millennia ya serikali ya chama tawala  ndiyo maana ulianzishwa mpango wa kuboresha elimu ya msingi MEM na kuboresha elimu ya sekondari MES.

Hata hivyo mpango wa kuboresha elimu bora kwa watanzania unaonekana kukabiliwa na changamoto nyingi katika baadhi ya maeneo yenye mazingira magumu kama hali ilivyo katika shule ya msingi Darpori iliyopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma. Mwenyekiti wa kijiji cha Darpori Andason Haule anasema kijiji hicho chenye utajiri wa madini ya dhahabu kina watu karibu 10,000 kilianza rasmi mwaka 2004, kina karibu makabila yote 120 yaliopo nchini pamoja raia kutoka nchi jirani za Malawi na Msumbiji. Read the rest of this entry

Ugonjwa wa kifafa washambulia kijiji kizima

Standard

   Picha inamunesha mwanafunzi wa shule ya msingi Mtua iliyopo katika kata ya Mpepai wilayani Mbinga mkoani Ruvuma akiwa ameungua moto.Mwanafunzi huyu anasumbuliwa na ugonjwa wa kifafa,alipata ajali ya moto baada ya ugonjwa huo kumuanza akiwa hata mwangalizi hivyo kuangukia kwenye moto

Na Albano Midelo

Wananchi wa Kijiji cha Mtua ambacho kinapakana na pori la wanyamapori la Liparamba wilayani Mbinga mkoani Ruvuma wapo katika hatari baada ya ugonjwa wa kifafa kushambulia karibu kijiji kizima.

Uchunguzi umebaini kuwa  katika kijiji hicho chenye wakazi zaidi ya 1600 watu 200 wanadaiwa wanaugua kifafa ambapo kila nyumba kuna mgonjwa mmoja wa kifafa na baadhi ya nyumba zina wagonjwa wawili hadi watatu hali ambayo inasababisha wananchi wa kijiji hicho kuhitaji msaada mkubwa kutoka wizara ya afya na ustawi wa jamii kwa lengo la kukinusuri kijiji hicho. Read the rest of this entry

Ubovu wa barabara wasababisha nauli kufikia 40,000

Standard


Picha inawaonesha wasafiri wanaotoka wilayani Mbinga kwenda kijiji cha Darpori kilichopo mpakani  mwa Tanzania na Msumbiji  ambao licha ya kulipa nauli ya shilingi 40,000 pia wanakaa juu ya magari au kushika bomba kama wanavyoonekana katika picha  

  Na Albano Midelo.

UBOVU wa barabara  yenye urefu kilometa 82 kutoka wilayani Mbinga hadi katika kijiji cha Darpori kilichopo mpakani mwa  nchi za Tanzania na Msumbiji kumesababisha abiria kulipa nauli kati ya shilingi 30,000 hadi 40,000.

Uchunguzi ambao umefanywa na mwandishi wa habari hizi  umebaini kuwa wananchi wanaoishi katika kijiji hicho na kilichopo katika kata ya Tingi wanakabiliwa na matatizo makubwa yanayotokana na tatizo sugu la ubovu wa barabara. Read the rest of this entry

Mwekezaji apora eka 5000 za wananchi

Standard


Picha inaonesha baadhi ya wakulima katika kijiji cha Lipokela wilayani Songea wakivuna mahindi yao baada ya kuwaambiwa kuwa mashamba hayo sio mali yao ni mali ya mwekezaji hivyo wanatakiwa wayavune haraka.

Na Albano Midelo

WAKAZI wa kijiji cha Lipokela wilayani Songea mkoani Ruvuma  wanamuomba waziri wa ardhi,nyumba na maendeleo ya makazi  Profesa Anna Tibaijuka kuwasaidia kuirejea ardhi yao yenye ukubwa wa zaidi ya eka 5000  iliyochukuliwa kinyemela na mwekezaji.

Wakizungumza na waandishi wa habari katika kijiji hicho baadhi ya wananchi walidai kuwa  mwekezaji mwenye asili ya Asia anayefahamika kwa jina moja la Merali  tangu mwaka 1985 alipewa ardhi kinyemela bila Baraka za wananchi na kusababisha ardhi hiyo kuingia kwenye mgogoro mkubwa. Read the rest of this entry