Monthly Archives: July 2011

Mimba zinavyotishia elimu kwa wanafunzi Ruvuma

Standard

Na Albano Midelo.

 JUMLA ya wanafunzi 554  wamepata mimba katika mkoa wa Ruvuma katika kipindi cha kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka jana. Mkuu wa mkoa wa Ruvuma Dr.Christine Ishengoma alibainisha kuwa kati ya waliopewa mimba  wanafunzi wa shule za msingi ni 283 na sekondari 271.

Takwimu hizo zinaonesha kuwa kati hao waliopewa mimba wilaya ya Mbinga wanafunzi 114 wakiwemo wa shule za msingi 15 na sekondari 99 walitiwa mimba ambapo kesi tatu zipo mahakamani na kesi 111 zipo katika ofisi za watendaji wa vijiji.Wilaya ya Namtumbo wanafunzi 148 ,kati ya hao wanafunzi wa shule za msingi 106 na sekondari 42 ambapo mahakamani zipo kesi 21,polisi kwa ajili ya upelelezi zipo kesi 28,ofisi za watendaji wa vijiji kesi 43 na kesi 14 zipo katika ofisi za watendaji wa kata. Read the rest of this entry

Advertisements

ICD na uimarishaji wa elimu jumuishi Tanzania

Standard
Picha inamuonyesha Afisa elimu wa manispaa ya Songea mkoani Ruvuma Fulgence Mponji akifungua moja ya mikutano muhimu ya wadau wa elimu mjini Songea.
  Na Albano Midelo.                .NI ukweli usiopingika kuwa elimu ni haki ya msingi kwa kila mtanzania pasipo kubagua uwezo,jinsia ama namna mtu anavyoonekana.Hata hivyo haki hii inaweza isitolewe kikamilifu kwa baadhi ya makundi kama vile watu wenye ulemavu pale ambapo mazingira ya upatikanaji wa haki hiyo yanapokuwa magumu.Takwimu za shirika la umoja wa kimataifa la kuhudumia watoto(UNICEF) zinaonesha kuwa ni asilimia 98 ya watoto wenye ulemavu katika nchi zinazoendelea ikiwemo Tanzania hawapati kabisa elimu.

Asilimia hiyo ndogo inachangiwa na kuwepo kwa shule chache maalum hapa nchini kwa ajili ya watu wenye ulemavu,ukosefu wa wataalum,sera na sheria za nchi zinazosimamia sekta ya elimu moja kwa moja na kutoa utaratibu mzuri wa kutoa kuhusu wenye ulemavu,ukosefu wa vifaa maalum na muhimu vya kuwawezesha kusoma pamoja na miundo mbinu duni katika shule zilizopo na vyuo isiyotosheleza na kukidhi mahitaji maalum ya watu wenye ulemavu. Read the rest of this entry

Uwindaji wa kitalii wauingizia mkoa wa Ruvuma milioni 890

Standard

Pichani hizi ni pembe mbili za ndovu ambazo uzito wake kwa pembe moja ni zaidi ya kilo 85 ambazo watalii wanazinunua kwa fedha nyingi na kuleta mapato makubwa yanayotokana na sekta ya utalii nchini.

 Na Albano Midelo

 SEKTA ya utalii katika kanda ya kusini bado haijapewa kipaumbele kikubwa kama ilivyo katika mikoa ya kaskazini na mikoa ya kanda ya mashariki.Mikoa ya kusini ambayo ni Ruvuma,Mtwara na Lindi ina vivutio vingi na vya kipekee vya utalii ambavyo bado havijatangazwa na hivyo kufahamika ndani na nje ya nchi.

Hata hivyo miaka ya hivi karibuni katika mkoa wa Ruvuma kunafanyika uhamasishaji wa kuvitangaza vivutio mbalimbali vya utalii na hivyo kuanza kufungua milango ya utalii kwa kuanza kupokea watalii ambao wanafurahia sana vivutio hivyo.Mkoa wa Ruvuma una mapori ya wanyamapori  katika wilaya ya Mbinga ambako kuna mapori ya Liparamba na Litumbandyosi ambayo yana msitu mnene wa asili ambao ni kivutio pekee licha ya kuwepo kwa wanyama,ndege na samaki.

Licha ya mapori hayo wilayani Mbinga,pia katika wilaya za Songea,Namtumbo na Tunduru kuna vivutio mbalimbali yakiwemo makumbusho ya mashujaa wa Majimaji,mapango,mawe na maeneo yanayofaa kwa uwindaji wa kitalii.Hadi sasa tayari mkoa wa Ruvuma umeshaanza kunufaika na uwindaji wa kitalii ambao unafanyika katika wilaya Songea ,Namtumbo pamoja na wilaya nyingine. Read the rest of this entry

Watu 800 waliuwawa katika jiwe la Litembo wilayani Mbinga mwaka 1902

Standard

Picha inaonesha jiwe la Litembo lililopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma.Jiwe hili lina utajiri wa utalii wa kishujaa na kihistoria kutokana na mababu  na mabibi zetu takribani 800 waliuwawa na wakoloni wa kijerumani mwaka 1902 katika vita ambavyo walikataa kutawaliwa na mkoloni.Jiwe hili linaitwa Litembo kutokana na kufanana sana na mnyama tembo.Kijiji cha Litembo pia kimepewa jina la jiwe hili ambalo pia lina pango refu ambalo mababu zetu walionusurika kwenye vita hivyo waliingia kwenye pango na kutokea upande wa pili  wa jiwe hilo picha na maelezo na Albano Midelo