Mashine mpya aina ya ABC ambayo ilitolewa katika ahadi za Rais Jakaya Kikwete tayari imefungwa kwa lengo la kupunguza tatizo la umeme mjini Songea.Mashine hiyo ina uwezo wa kuzalisha megawati 1.6
Na Albano Midelo
UBOVU wa mashine tatu kati ya sita za kuzalishia umeme katika kituo cha TANESCO mjini Songea mkoani Ruvuma umesababisha mgawo mkali wa umeme kwa wakazi wa mji huo.
Uchunguzi umebaini kuwa mgawo wa umeme umesababisha kazi za kiuchumi kushindwa kufanyika na kusababisha baadhi ya wananchi wenye uwezo kuamua kutumia majenereta madogo huku maeneo mengi ya mji wakati wa usiku yakiwa giza kwa saa kadhaa. Read the rest of this entry
Mwanaharakati Fatuma Misango katikati akisikiliza baadhi ya wanawake wakielezea ukatili wanaofanyiwa na wanaume zao.



Picha inakionesha kijiji cha Darpori kilichopo wilayani Mbinga mkoani Ruvuma,kijiji hiki kina watu 10,000 kipo mpakani mwa nchi za Tanzania na Msumbiji,tangu uhuru hadi sasa kijiji hiki licha ya kuwa na utajiri wa milima yenye dhahabu na idadi kubwa ya watu hakina huduma yeyote ya afya hali ambayo inaathiri ustawi wa jamii ikiwa ni pamoja na watu kupoteza maisha.